Alhamisi 22 Oktoba 2026 - 17:50
Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza/ Hawza ya Ahlulbayt, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Dar-ul-Muslimi'na, iliyopo Dodoma, Tanzania, imefanya mahafali ya watoto waliohitimu mafunzo yao ya kidini, ikiwa ni hatua muhimu katika kuwajengea msingi imara wa maarifa ya Kiislamu na kuwaandaa kuendelea na masomo yao katika ngazi za juu zaidi.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mahafali hayo yamefanyika tarehe 20 Oktoba 2026, chini ya usimamizi wa Haaj Muslim Banji, huku yakionesha juhudi zinazoendelea kufanywa na Hawza hiyo katika kuimarisha elimu ya dini miongoni mwa watoto na kuwalea katika misingi na mafundisho ya Uislamu.

Hawza ya Ahlulbayt ina utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo ya kidini kwa watoto kwa muda wa miaka minne, baada ya kukamilisha kipindi hicho cha mafunzo, wanafunzi huhitimu na kupata fursa ya kuendelea na masomo yao katika ngazi za juu zaidi, hatua inayolenga kupanua uelewa wao wa mafundisho ya dini na kuimarisha maarifa yao ya Kiislamu.

Mpango huu una nafasi muhimu katika kuwahamasisha watoto kupenda elimu ya dini tangu wakiwa katika umri mdogo, kuwajengea maadili mema na kuwasaidia kukua wakiwa na uelewa mpana wa mafundisho ya Uislamu. Aidha, jitihada hizo zinaonesha umuhimu wa kuwekeza katika malezi na elimu ya kidini kwa kizazi kipya ili kiweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha kwa kuzingatia maadili na misingi ya Kiislamu.

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Hawza ya Ahlulbayt Dodoma Yafanya Mahafali ya Watoto Waliohitimu Mafunzo ya Kidini

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha